Imeripotiwa kuwa milio ya risasi ilisikika nyumbani kwa Rapper Lil
wayne huko Miami beach siku ya jana,Polisi walipokea simu kuwa kuna
milio ya risasi nyumbani kwa rapper huyo na inawezekana watu wanne
wanaweza wakawa wamepigwa na risasi kutokana na tukio hilo.
Baada ya polisi kufika eneo la tukio, walisema kuwa taarifa zilikua
za uongo na hakuna mtu yoyote aliyepigwa risasi. Mtandao wa TMZ
umeripoti kuwa Lil wayne hakuepo nyumbani wakati wa tukio hilo, Pia
Manger wa rapper huyo,Cortez Bryant aliuambia mtandao wa XXL kuwa “Wayne
was never home he was in the studio working. It was a prank call to the
police on the 911 line that alerted them to go to the property. I
allowed them access in and they found the house empty. All is good”
No comments:
Post a Comment