Mastaa wa Bongo Fleva,Q-Chillah na TID mwishoni mwa wiki hii walitaka kutwangana walipokutana katika Klabu moja usiku.
Kwa mujibu wa Q-Chillah akizungumza kwenye Uheard na Soudy Brown alisema kuwa alikwenda kwenye klabu hiyo kuangalia shoo iliyokuwa ikifanyika lakini baadaye aliamua kutoka nje kucheza ‘pool table’ ndipo alipomuona TID.
‘’Nilimuona jamaa(TID) akiniangalia na baadaye alinifuata akaniambia
kuwa anataka kuongea na mimi nikamwambia ile siye sehemu yake atafute
muda mwingine ndiyo tuongee,’’alisema Q-Chillah.
Aidha Chillah aliongeza
kuwa TID aliendea kumuongelesha ndipo alimwambia kuwa anachofanya
kumuongelea yeye vibaya siyo vizuri na kile alichokipost hivi karibuni
kuhusu kuuponda wimbo mpya wa msanii Ali Kiba uitwao ‘Cheketua’
aliouachia hivi karibuni kupitia account yake ya Instagram hakikuwa kitu
cha busara ilitakiwa amsapoti kama msanii mkongwe kuliko kumponda
hadharani kupitia mitandao.
‘’Kiukweli kitendo cha TID kuandika Instagram kuwa ngoma mpya ya Alikiba
ni mbaya na baada ya miezi mitatu haitokuwepo siyo kizuri nilimwambia
yeye ni msanii mkubwa inabidi kumsapoti Ali Kiba na kwamba nilitaka
kumpiga kwa fimbo ya pool table siyo kweli nilikuwa nikimueleza
tu,’’aliongeza Q-Chillah.
No comments:
Post a Comment