Muimbaji huyo ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki amezungumza na Kikwetu Blog na kutaja mambo muhimu ambayo wasanii wakongwe kama yeye wanatakiwa kuzingatia ili kukabiliana na changamoto kutoka kwa wasanii wapya na pia kuendelea kufanya vizuri.
Jambo la kwanza aliloshauri ni wasanii hao kukubaliana na ukweli kuwa muziki umebadilika na kwamba wawe tayari pia kuyapokea mabadiliko hayo.
Mimi nimekubaliana na changamoto na ndio maana naenda vizuri naenda sawa na vijana, naenda sawa na watu wa rika langu,” amesema.
Kiukweli kabisa kama utaamua kuvaa vazi la mwaka 2000 ukavaa mwaka 2015 hutaweza kuwa wa kisasa. Lakini kama utavaa vazi la 2015 na utaimba muziki wa 2015.”
Dully ameongeza kuwa kitu kingine muhimu wasanii wakongwe wanakosea ni kutojihusisha na mitandao ya kijamii na hivyo kuwafanya mashabiki wasijue wanachokifanya.
No comments:
Post a Comment