16 February 2015

Muziki wa Tanzania wazidi kung’ara, Vanessa, Diamond na Shaa washika chart kubwa za kimataifa

Muziki wa Tanzania unaendelea kufanya vizuri zaidi kimataifa.

Nyimbo za Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Shaa na Navy Kenzo zinafanya vizuri kwenye chart za vituo vya runinga vya kimataifa.


Wimbo wa Diamond Platnumz, Ntampata Wapi wiki hii umekamata nafasi ya tatu kwenye chart ya nyimbo 30 zinazofanya vizuri barani Afrika na duniani kwenye kituo cha Ufaransa cha Trace Urban. Pia wimbo huo unatambulika kama Smash Hit kwenye kituo hicho.

Kwa upande wa wimbo wa Vanessa Mdee, Hawajui, wimbo huo Jumapili hii umekamata nafasi ya tano kwenye chart ya nyimbo tano bora ya Trace Urban iitwayo Top Music.

Hawajui pia imekamata nafasi ya tano kwenye chart ya Access 20 Live inayoandaliwa na kampuni ya Think-Tank Media ya Afrika Kusini.

Wimbo wa Shaa ‘Njoo’ aliomshirikisha msanii wa Kenya Redsan umeendelea kufanya vyema kwenye chart za kituo cha Nigeria cha Sound City huku Navy Kenzo nao wakiendelea kuwepo kwa wimbo wao ‘Moyoni’.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname