HABARI ya mjini ni kwamba, lile penzi linalonadiwa la Mbongo-Fleva,
Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na mwigizaji Wema Isaac Sepetu ‘Madam’
limejaa magumashi, ikidaiwa kuwa jamaa huyo kawekwa kama boya tu, nyuma
yake kuna kigogo mzito serikalini ndiye anayekula vinono.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Dimpoz ameagizwa na kigogo huyo awe
mpenzi kivuli wa Wema ili kuzuga watu wasishtukie mchezo kama yeye ndiye
anayesukuma gududumu la malovee kwa Madam.
“Kutokana na unyeti wa kazi yake, jamaa hataki kujitokeza ‘front’ ndiyo
maana ameamua kumtumia Dimpoz kama kanyaboya huku yeye akiendelea kula
vyake,” kilisema chanzo hicho.Kikizidi kumwaga ubuyu, chanzo hicho
kilidai kigogo huyo ndiye anayedhamini safari zote za Wema na Dimpoz nje
ya nchi ikiwemo ile ya juzikati nchini Marekani ambayo ilibuma.
“Jamaa ana pesa chafu, amemnunulia Wema viwanja viwili kimoja kipo
Tabata na kingine Kigamboni, Dar, ndiye anayemwezesha Wema katika
shughuli zake za kila siku.“Kigogo huyo ndiye chanzo cha Wema kummwaga
Diamond, alimpotezea kwa sababu ya maslahi zaidi, hata kwenye bethidei
ya Wema mwaka jana, kigogo huyo ndiye aliyegharamia vitu kibao hadi
kusababisha Diamond ahoji,” kilisema chanzo chetu.
Jitihada za kumsaka kigogo huyo ili azungumzie ishu hiyo hazikuzaa
matunda lakini alipotafutwa Dimpoz na kusomewa tuhuma hizo,
alijibu:“Watu watambue kuwa uhusiano wangu na Wema upo kwa ajili ya
‘project’ zangu, niacheni please niinjoi maisha yangu kuhusu huyo kigogo
muulizeni vizuri Wema mwenyewe,” alisema Dimpoz.
Mwanahabari wetu alipomvutia waya Wema, alijibu kwa kifupi na kukata simu:
“Ujue sasa hivi mimi sitaki malumbano na mtu, najua kila mtu siku hizi
anaongea kila anachojisikia, naomba niachwe na maisha yangu, unayoyasema
hayana maana, wanasema kwa sababu hakuna anayemjua mpenzi wangu wa
sasa sina muda wa kubishana.”
Hivi karibuni, wakiwa Sauz, Wema na Dimpoz, picha zao wakiwa kimahaba
zilivuja mitandaoni hivyo kuibuka gumzo kuwa huenda kwa sasa nao
wanatoka.
Credit GPL
No comments:
Post a Comment