Linah amekiri kuwa tangu ayajue mapenzi, hajawahi kumpata mwanaume aliyempa mapenzi ya kweli.
Akiongea kwenye kipindi cha Funiko Base cha Radio 5, Linah ambaye hivi
karibuni aliachia ngoma mpya ‘Hello’ aliyoshirikiana na Christian Bella
amedai kuwa ndio maana amekuwa akiimba ujumbe kama huo kwenye nyimbo
zake.
“Lakini sasa hivi nimepata mapenzi ya kweli,” amesema.
“Sijawahi kukaa kwenye mahusiano kwa zaidi ya miaka mitatu lakini sasa nimekaa kwenye mahusiano kwa miaka mitano,” ameongeza.
No comments:
Post a Comment