16 February 2015

Huyu ndie Mwnafunzi aliyeongoza kufanya Vizuri Tanzania Nzima Matokeo ya Kidato cha Nne (4) Mfahamu Zaidi Hapa

Nyakaho Marungu (16) Mwanafunzi bora wa mihani wa kidato cha nne mwaka 2014,Nyakaho Marungu (16),amesema mazingira mazuri ya kusomea na msaada anaoupata kutoka wa wazazi wake ndiyo uliofanikisha afike hapo halipo
 
Marungu mkazi wa kitunda alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na NIPASHE jumapili na kuelezea kuwa,ufaulu huo pia ulitokana na umakini wakekatika masomo.
Mwanafunzi huyo ambae anasoma katika shule ya Sekondali Baobab iliyopo Bagamoyo Mkoani Pwani,amekuwa wa kwanza kati ya wanafunzi 196,805 waliofanya mtihani huo mwaka jana baada ya kuibuka na ponti 5.1 "Nilitarajia kufanya vizuri lakini sikujua kama nita kuwa mwanafunzi bora wa mwaka 2014 nchi nzima" alisema
  
Nyakaho ambaye wakati wote alionyesha uso wa furaha akiwa nyumbani kwa wazazi wake alisema anawashukuru wazazi wake,Walimu na mazingira mazuri ya shuleni yaliyomfikisha hapo"Jitihada binafsi kujituma kusoma kwa bidii hasa wakati wa usiku,pia uwepo wa vifaa vyakutosha Shuleni pamoja na vitabu vimenisaidia sana"alisema na kuongeza Shule ina vifaa vya kutosha ikiwa ni pamoja na maabara nzuri ya kisasa na kuongeza pia anapendelea kusoma masomo ya sayansi"alisema wakati wote akiwashuleni alitumia muda mwingi kujisomea masomo ya sayansi"alisema wakati wote akiwa shuleni alitumia muda mwingi kujisomea kwa kuwa aliamini mafanikio hayapatikani bila kujituma".Mama wa mtoto huyo Selestina Maro,alisema Nyakaho ni mtoto wake wapili na kwamba mafanikio yake yanatokana kwa jitihada zake binafsi."Darasa la saba alifaulu na kwenda shule ya sekondari ya Jangwani lakini tuliamua kumpeleka St.Thereza iliyopo Arusha ambapo huko alisoma kw amwka mmoja,shule ya Baobab alianzia kidato ca pili hadi akamaliza"alisema na kuongeza
"Ushauri wang kwa wazai na walezi wafuatilieni watoto wenu wanapotoka likizo au wanaporudi kutoka shule siyo kuangalia televisheni,hakikisheni wanakazania masomo"alisema

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname