Mchezaji wa zamani wa timu ya Bayern Munich na timu ya Taifa ya Ghana Samuel Osei Kuffour ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka katika kituo cha television cha Super Sport, amenyoa nywele zake baada ya timu ya Taifa ya Ghana kufungwa kwa changamoto za mikwaju ya penati kwenye fainali ya AFCON 2015.
Kuffour alitabiri kuwa Ghana wangeibuka na ushindi katika mechi ya fainali dhidi ya Ivory Coast na kama wasiposhinda basi anyolewe nywele zake.
“Mleteni kabisa kinyozi kwenye jumba hili kubwa, ili Ivory Coast wakishinda aninyoe nywele zangu zote,” Kuffour alisema kabla ya mechi kuanza.
Na baada ya mechi kumalizika na Ivory Coast kushinda kwa penati 9-8 dhidi ya Ghana ndipo mtangazaji mmoja akachukua mashine ya kunyolea na kuanza kunyoa Akuffour
No comments:
Post a Comment