Awali
Ijumaa Wikienda lilipokea taarifa juu ya kuumwa kwa Banza ambapo
ilielezwa kuwa, alilazimika kusafirishwa kutoka Mbeya hadi Dar baada ya
hali yake kiafya kuwa mbaya.
Maskini!
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza
Stone’ yu mgonjwa tena, safari hii ameibuka na kueleza maradhi ambayo
yanamsumbua akisema: ‘Ugonjwa huu
utaniua.”AJIKONGOJA
utaniua.”AJIKONGOJA
Hivi
karibuni, gazeti hili lilimfuata nyumbani kwake Sinza ya Vatican jijini
Dar na baadaye alijikongoja na kwenda kwenye Ukumbi wa Flamingo uliopo
Magomeni ndipo akazungumzia kinachomtesa.
KICHWA
Banza ambaye siku hizi hupenda kujiita Roho ya Paka alisema kuwa kinachomsumbua ni maumivu ya kichwa hasa wakati wa jua kali.
KIZUNGUZUNGU
“Kichwa
kinaniuma sana hasa wakati wa jua kali, mishipa ya kichwa inaniuma sana
halafu nasikia kizunguzungu muda wote, sifahamu ni kwa nini,” alisema
mwanamuziki huyo akionekana kuwa na maumivu makali.‘Banza Stone’ akiuguza ugonjwa.
Jamaa huyo alisema kuwa anaendelea na tiba akisaidiwa na mama yake, Hadija.
“Kwa
sasa nipo tu nyumbani, natazama afya yangu, ukweli nahitaji matibabu ya
nguvu ili kunirejesha kwenye hali yangu ya kawaida,” alisema Banza.
MSAADA WA MADAKTARI
Hata
hivyo, Banza alisema hataki kuomba msaada wa kuchangiwa fedha ili
kupata matibabu ila anachoomba ni madaktari ambao wanafahamu tiba ya
ugonjwa huo ili wamsaidie kimatibabu.
Si mara ya kwanza kwa Banza kuumwa kwani mara kadhaa alisharipotiwa kuwa hoi kwa magonjwa mbalimbali ikiwemo kifua.
KUTOKA KWA MHARIRI
Ijumaa
Wikienda linamtakia Banza afya njema ili arejee jukwaani kuwapa
burudani mashabiki wake na madaktari wanaoona wanaweza kumtibu,
wajitokeze.
No comments:
Post a Comment