09 February 2015

BARCELONA FC WANAKUJA BONGO NA WATACHEZA TAREHE 28/3/2015 UWANJA WA TAIFA NA NYOTA WATANZANIA SOMA HAPA


 Mshambuliaji wa zamani wa FC Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi Patrick Kluivert alizungumzia ujio wa magwiji FC Barcelona nchini mwezi wa tatu mbele ya waandishi wa habari kwenye mgahawa wa Sports Lounge uliopo jijini Dar Es Salaam ,Pembeni ya Kluivert ni mwenyekiti wa DRFA Ndugu Almas Kasongo. Magwiji hao wa Barcelona wanataraji kucheza na wachezaji nyota wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa mnamo mwezi wa machi tarehe 28. 
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Dar Es Salaam,Almasi Kasongo akizungumza kwenye mkutano huo katikati na mwakilishi wa FC Barcelona pamoja na Mwakilishi wa kampuni ya Prime Time Promotions Stuart Kambona ambao ni waratibu wa mchezo huo.
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo mapema leo asubuhi

Timu ya wachezaji nyota wa zamani wa Barcelona FC watacheza na wachezaji wa zamani wa Tanzania, Tanzania All Stars Machi 28 kwenye uwanja wa Taifa jijini.Mwakilishi wa wachezaji wa zamani wa Barcelona, Patrick Kluivert alisema jana kuwa mechi hiyo itawahusisha wachezaji nyota wa Barcelona wakiwemo, Edgar Davids, Gaiza Mandieta, Ludovic Giuly, Francesco Coco na wengine wengi waliopitia klabu hiyo kwa miaka tofauti.Kluivert alisema kuwa kikosi chao kina wachezaji nyota ambao ni maarufu duniani na wanaamini mechi itakuwa nzuri na yenye ushindani mkubwa.

Alisema kuwa yeye ni mwenyeji sana hapa Tanzania kwani huu ni ujio wake wa tatu na anaamini kuwa jinsi mashabiki wanapenda sana mpira wa miguu, itakuwa fursa kubwa kwao kuona vipaji vya zamani ambavyo  vimetukuka.“Ninafurahi kuja nchini Tanzania kwa mara ya tatu, ni faraja kubwa pia kucheza hapa nchini kwa mara ya kwanza, naomba mashabiki wa soka wajae uwanjani kuona mpira wenye ushindani,” alisema Kluivert.

Mwakilishi wa kampuni ya Prime Time Promotion inayoratibu mechi na ziara ya timu hiyo ya Barcelona, Stuart Kambona alisema kuwa madhumuni ya mchezo huo ni kudumisha mahusiano ya kibiashara ya mpira wa miguu baina ya Tanzania na Hispania, kutangaza utalii na kuendeleza mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili.

Kambona alisema kuwa pamoja na kucheza soka siku hiyo, ujio wao pia utaitangaza nchi nje ya mipaka yake na kuleta fursa nyingi hapa nchini.“Wachezaji wa Barcelona wanataingia nchini siku mbili kabla ya mechi na watakuwa zaidi ya 20, majina ya wachezaji wengine yatatangazwa baadaye, ila tunaomba wadhamini wajitokeze kufanikisha na kufaidika na  mechi hiyo,” alisema Kambona.

Mwenyekiti wa Chama cha soka cha mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)  Almasi Kasongo aliwaomba mashabiki wa soka kujiandaa kuangalia mechi hiyo  kwa kufika uwanjani.

Kasongo alisema kuwa DRFA imefarijika sana kwa ziara hiyo na kuiomba Prime Time Promotion kuhakikisha kuwa inapanua wigo kwa kuandaa mechi nyingi ambazo zitakuwa chachu ya maendeleo ya soka nchini.
 
Source: Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname