16 February 2015

BREEKING NEWS-SAMWEL SITTA AMSIMAMISHA ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU WA BANDARI



Pichani Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Bandarini aliyesimamishwa kazi Maden Kipande
HABARI iliyotufika mda huu zinasema Waziri wa Uchukuzi Samwel Siita amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Maden kipande kutokana na matumizi mabaya ya ofisi yaliyopelekea hasara serikali ya mabilioni ya shilingi,
Kusimishwa huko kwa Mkurugenzi Kipande kunatokana na Jitahada kubwa kati ya Vyombo mbalimbali vya Habari ikiwemo mtandao huu kufichua ufisadi uliokuwa unafanywa na Mkurugenzi huyo bandarini ikiwemo huu hapa ANAANDIKA. KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kwa Mujibu wa vyanzo vya kuaminika kutoka katika Mamlaka hiyo ambayo ni kitovu cha Maendeleo ya Nchi yetu ambazo mwandishi wa mtandao huu amezipata ,zinasema mkurugenzi huyo amekuwa akiwasimamisha wafanyakazi kinyume na Taratibu na sheria.

Chanzo hicho kinasema mkurugenzi huyo,amekuwa akiwasimamisha watu tu pasipo kuwa na kosa lolote kwa mfano mwishoni mwa mwezi uliopita ameanzisha Mpango wa kumngoa Meneja wa Bandari ya Tanga,Hassani Kyomile eti akisema Meneja huyo amekuwa akivujisha siri kwenye Gazeti moja la wiki akidai Mhariri wa Gazeti hilo ni Mhaya ,na meneja huyo pia ni mhaya eti anavujisha siri kwenye Gazeti hilo,ambapo kipande anaona kumfukuza meneja huyo kutarahisisha mipango yake ya kifisadi pasipo kuvuja.

Pichani ni Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta picha na maktaba
Chanzo hicho kilizidi kusema Kipande amekuwa akijivunia kwa Wanyakazi wake kwamba anaweza kufanya lolote na hakuna wakumzuia,ambapo amesimamisha watu kazi zaidi ya miaka miwili huku wakiwa wakipokea mishahara pamoja na malupulupu huku wakiwa nyumbani bila hata ya kufanya kazi.Chanzo hicho kiliwataja wafanya kazi hao,miongoni mwao ni Mama Muhindi,ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Masoko TPA,ambaye alisimamishwa kazi na Kipande kwa Madai alikuwa anavujisha siri(madudu)za TPA kuhusu kwenye vyombo vya Habari,licha ya mkurugenzi kipande alishindwa kutokea wala kukanusha kwenye vyombo vya Habari juu ya Ufisadi huo ,
Tuhuma,zinginene zinazozidi kumkabili kipande kuhatarisha usalama wa Bandarini kwa kutokuna na kutokuwepo na Kamera CCTV pamoja na mita za kupima mafuta yanayoingia nchini kutokafanya kazi kwa miaka mitatu sasa.
Jambo la kushangaza Mama huyo Muhindi,alisimaishwa kazi tangu agosti 2013 na kipande,lakini hajahojiwa wala kurudishwa kazini ,huku akizidi kuendelea kuchukua mshahara na Marupumarupu mengine bila kufanya kazi hadi sasa wala hajahojiwa na mamlaka yeyote.
Chanzo,hicho kilizidi kutaja orodha ya Wafanyakazi walionewa na Kipande ambae ni Mfanyakazi mwingine ndugu Msemo,aliyekuwa Afisa Ununuzi,naye alisimamishwa kazi tangu agosti2013 kwa tuhuma zisizokuwa za Ukweli wowote, lakini mpaka sasa naye anaendelea kuchukua mshahara pamoja na marupurupu yote pasipo kufanya kazi.
Waliosimamishwa na kipande kwa tuhuma hewa
Hery Arika,aliyekuwa Men eja Biashara wa Bandari ya Dar es Salaam,alihamishiwa makao makuu na kuambiwa kuripoti idara ya utawala tangu April 2013 hadi leo hii,Analipwa mishahara na marupurupu yake bila kufanya kazi kwa mwaka mmoja sasa,kwa madai ya Kipande hamtaki.
Ajira za Upendeleo,
Kama kuna mgogoro unaofuka Moshi Ndani ya Bandari basi ni huu unaotokana na Ajira za Mhandisi Alois Matei,ambaye ni Naibu Mkurugenzi mkuu(Maendeleo ya Miundombinu)na mhandisi William Shilla,ambaye ni mkurugezni wa Uhandisi.Taharifa zilizopo zinasema kuwa Wahandisi hawa wawili waliajiriwa na Kipande kupitia Mlango wa Nyuma ,pasipo kufuata taratibu za sheria.
Huu ni Mwenderezo wa Unyama unaofanywa na Kipande ndani ya Bandari pasipo kuchukuliwa Hatua yeyote kutoka kwenye Taasisi za Kupambana na Rushwa TAKUKURU,wala Wizara husika ya Uchukuzi ambao,mamlaka hiyo iko chini yake.
Huku,Kipande akinijinadi kwenye mkutano na Uongozi wa mamlaka hiyo,akisema mtu yeyote atakaye pingana nae anamngoa kwani yeye na mamlaka hiyo ya Bandari hawapati hasara yeyote bali serikali ndio inapata hasara,na kama yuko mtu yeyeto atakaye pingana naye(Kipande )basi atamfukuza Kazi.
Duru, hizo zinasema mzee Kipande amekuwa akifanya Vitendo hivyo vya Kifisadi huku akijinadi Hakuna mtu wa kumng”oa nafasi hiyo kwa Madai,eti anajuana Kigogo mmoja aliyoko Ikuru ya Jakaya Kikwete,ambae amekuwa karibu na Kipande.Ndio maana Amekuwa akifanya Vitendo hivyo akijua hakuna mtu wakumchukulia Hatua zozote

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname