19 February 2015

Alichokisema Wabogojo baada ya kukamatwa na askari Hong Kong akizaniwa kubeba madawa ya kulevy

http://www.bongoclantz.com/Sote tunajua kua kwa sasa jina la Tanzania limechafuliwa baada ya watu wengi kukamatwa nchi mbalimbali ikiwemo china wakisafirisha madawa ya kulevya. Hali hiyo imesababisha raia kutoka Tanzania mara waingiapo katika baadhi ya nchi kukaguliwa sana kuangalia kama wamebeba madawa ya kulevya au la.

Jana kupitia Instagram Star Wabogojo aliyetamba miaka ya mwanzoni mwa 2000 kwa kuonekana katika Video ya Mr Nice alipata adha hiyo ya kukaguliwa na askari wa Hong Kong China wakumhisi kua kabeba madawa ya kulevya.

Wabogojo aliandika " 18022015 Hong Kong Mapumziko
ASANTENI KWA KWA KUNITAKIA MEMA KATIKA SIKU YANGU YA KUZALIWA..
ILA LEO WAKATI NAINGIA HONG KONG BODA WALIVYOONA TANZANIAN PASSPORT BASI NIKAPELEKWA KWENYE KACHUMBA.
NKASACHIWA SANA TU HUKU WAKINIHOJI KUHUSU SHOW YETU,,,KUMBE WANANIJUA LAKINI KUSACHI HAWAJAACHA.
ETI WANAIPENDA SHOW YETU NAMI NIKAWAAMBIA NAIPENDA FAMILIA YANGU UNGA SIBEBI LABDA SEMBE AU DONA ������������
NA TAMAA YA MAHERA MENGI SINA...
NILIKASIRIKA ILA SIO KOSA LAO KOSA LETU SISI WA TZ NA WAAFRIKA WENGINE.
JAMANI WAKIKUSHIKA NA UNGA HAWA JAMAA NI MIAKA TISA HIVI NDO WAMEKUONEA HURUMA."

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname