Siku hizi sio kitu cha ajabu kusikia au kuona wapenzi wamegombana na kufikia hadi kuachana kisa simu za mikononi.
Wapo wanaoishi kwenye dhana ya simu ya mkonomni ya mpenzi wako ni
simu yako na wapo wanaoishi kwenye dhana ya kila mtu na simu yake na
mambo yake hakuna kuchunguza simu ya mwenzio.
Mrembo na mwingizaji, Elizabeth Michael “Lulu” ameweka wazi mtanzamo
wake kuhusu simu ya mpenzi wake kwa kusema yeye hawezi kuipekuwa kwani
anaiona kama ni bomu.
Lulu aliandika hayo kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa INSTAGRAM
mara baada yakuweka picha ya mtoto akilia ikiwa na maadishi ya lugha ya
kingereza yakiwa na maana kuwa hiyo ilikuwa ni baada ya kupekua simu ya
mwanaume na kupata kile alichokuwa anakitafuta....
Lulu aliiandikia picha hiyo (tazama hapo juu);
“Hii inaitwa MWANA UKOME......Simu Ya Mwanaume naiona kama BOMU...!”
Wewe je simu ya mwenzi wako unaichukuliaje?
No comments:
Post a Comment