KATIKA hali ya kushangaza, polisi walijikuta wakipata shughuli pevu
kumkamata staa asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ambaye alidaiwa
kupiga muziki kwa sauti kubwa usiku kucha pasipo kuwa na kibali.
Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita, nyumbani kwa mwigizaji huyo,
Kijitonyama jijini Dar kulikokuwa na bethidei ya rafiki yake
aliyejulikana kwa jina moja la Neema.
Awali, mapaparazi wetu walipokea simu ya mmoja wa majirani wa Wema
ambaye alidai mwigizaji huyo amekuwa na tabia ya kufanya sherehe kwake
na kufungulia muziki mkubwa ambao unasababisha kero.
“Kwa kweli ni kero, kila mara amekuwa na tabia ya kupiga muziki mkubwa
katika sherehe zake ambazo hazina kichwa wala miguu. Kama jana (usiku wa
Jumatatu) muziki ulifunguliwa kuanzia saa mbili usiku mpaka asubuhi na
majirani walimfuata Wema mara kadhaa kumtaka apunguze sauti lakini
aliwajibu vibaya.
"Njooni mshuhudie wenyewe, tumeita polisi wamkamate,” alisema jirani mmoja.
Mapaparazi wetu walichukua usafiri wa pikipiki na kuwahi fasta na kukuta
polisi wakihangaika kwa muda mrefu kumkamata mrembo huyo lakini
ikashindikana kwa kuwa alikuwa amelewa na kukimbia hovyo huku akiwa nusu
utupu.
“Kwa sababu hiyo walimkamata mmiliki wa muziki ambaye jina lake
halikupatikana mara moja na mwenye sherehe (Neema) kisha kwenda nao
katika ofisi za mtendaji, Kijitonyama kwa ajili ya hatua za kisheria,”
alisema.
Akizungumza na gazeti hili, mwenyekiti wa mtaa huo, Mzee Haogwa,
alithibitisha kuletewa malalamiko ya Wema na kufika nyumbani hapo ambapo
pia alidai alishangazwa na kitendo cha kuwakuta wanaume tata kwenye
sherehe hiyo.
No comments:
Post a Comment