Rais Obama na Mkewe Michelle Obama,
wamefupisha ziara yao walipokwenda kutoa heshima zao katika familia ya
kifalme kwa kifo cha Mfalme Abdullah wa Soudi arabia kwani Michelle
Obama hakuwa na furaha pale walipofanya ziara ya kwenda kuutana na
mfalme mpya wa saudi arabia mfalme Salman.
habari zinasema kuwa Michelle Obama
hakuonekana kuwa na furaha kutokana na jinsi wanawake wanavyonyanyaswa
na mfumo dume lakini pia mapokezi aliyoyapata yeye hayakumfurahisha.
Inchi ya Soudi arabia ni nchi
ambayo wanawake hawaruhusiwi kutoka au kutembea hadharani bila kuvaa
ushungi, pia wanawake katika nchi hiyo hawaruhusiwi kuendesha gari yaani
ni marufuku kabisa kwa mwanamke kuonekana anaendesha gari lakini pia
wanawake hawaruhusiwi kabisa kuwa na akaunti benki na mambo mengine
mengi
Lakini pia Mrs Obama hakufurahishwa na
mapokezi, kwani waliposhuka kutoka ndani ya ndege walikutana na msafara
wamapokezi ulioongoza na viongozi wa Nchi hiyo, lakini ajabu katika
msafara huo ambao ni wanaume watupu, wengi wao walikuwa wakigoma
kusalimia kwa kumshika mkono.
habari zinasema kuwa wengi wa waliokuwa
katika msafara huo wakusalimiana na Rais Obama walikuwa wakikwepesha
mikono pale walipotaka kusalimiana na Michelle Obama na badala yake
kuishia kuinamisha vichwa tu.
Michele hakufurahishwa na kitendo hicho
kwani pamoja na kujitahidi kuvaa nguo ndefu iliyofunika miguu yake
lakini alionekana kama kavunja sheria ya nchi yao kwa kutokifunika
kichwa chake.
No comments:
Post a Comment