
Mwanamuziki
ambae ni dada na Diamond Platnum Queen Darleen amezidi kuchochea chuki
na bifu kwa mashabiki wa Ali Kiba na Diamond Platnum baada ya kupost
maneno ambayo mashabiki hao wanaona ni kama anazidi kuchochea bifu
iliyopo kwa mashabiki wa wanamuziki hao ambao kwa sasa wamekuwa na
ushindani mkubwa kimuziki.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita kulikuwa na show kubwa ya muziki ambayo ilifanyika
katika viwanja vya Ledears Club ambapo katika show hiyo iliwakutanisha
Diamond Platnumz pamoja na Ali Kiba ambao kila mmoja alipata mapokezi
tofauti kutoka kwa mashabiki wao.
Katika
show hiyo kuna baadhi ya mashabiki ambao walikuwa na furaha kushuhudia
show ya wakali hao wawili wakati show inaendelea msanii Diamond Platnum
aliweza kuwarushia noti za buku mbilimbli mashabiki wake.Kufuatia
kitendo hicho ndipo msanaii Queen Darleen amefunguka na kusema kuwa dawa
ya machupa stejini ni pesa. "Machupa kiboko yake pesaa,tunasaka hela na
wewe saka "
Mashabiki
wa Queen Darleen wameonyeshwa kutofurahishwa na kauli ambayo imetolewa
na dada wa nyota wa muziki Diamond Platnum na wao wanaamini kuwa msanii
huyo anazidi kuchochea bifu iliyopo kwa mashabiki wa Diamond pamoja na
Ali Kiba
No comments:
Post a Comment