22 January 2015

Makamba: Enzi za ushindi wa kishindo CCM zimepita


Siku chache baada ya matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuonyesha kuwa CCM, imeporomoka, Mbunge wa Bumbuli, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewataka wanachama wa chama hicho kujiandaa kisaikolojia kwa matokeo yoyote yanayoweza kutokea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.

“Wana-CCM wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwani walizoea ushindi wa asilimia 90 au 80 (wa kishindo), huu ulikuwa ushindi wa nyuma. Tusishangae tukipata ushindi wa asilimia 50, 60, 57 au 70 ni kitu cha kawaida kutokana na kukua kwa demokrasia hususan ushindani wa vyama vingi vya siasa kuanza kuimarika.

Kauli hiyo ya Makamba imekuja wakati matokeo ya serikali za mitaa yakionyesha kuwa CCM imeporomoka kutoka ushindi wa asilimia 91.7 mwaka 2009 hadi 79.8 katika uchaguzi wa mwaka jana na upinzani ukipanda kutoka asilimia nane mwaka 2009 hadi takriban 20 mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname