Jeshi la Polisi la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA)linamshikilia raia wa Kuwait kwa tuhuma za kukutwa na viumbe hai
aina ya Kenge 149 wenye thamani ya Sh 6.3 milioni.
Kamanda wa Polisi wa JNIA, Khamis Suleiman alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa
ni Hussain Ahmed Ally Mansour(34), raia wa Kuwait ambaye alikamatwa
uwanjani hapo jana majira ya saa 5 usiku wakati akijiandaa na safari
ya kuelekea nchini Kuwait kupitia Dubai na Shirika la Ndege la
Emirates .
Kamanda Selemani alisema Mansour alikamatwa na wanyama hao ambao
aliwahifadhi kwenye mifuko midogo midogo ilivyowekwa katika begi kubwa
lenye rangi nyeusi.
“Kenge waliwekwa kwenye mifuko midogo midogo 15 na kila mmoja kuna kenge
15 na mifuko mingine walikaa wawili,”alisema kamanda Selemani.
Alisema kati ya Kenge hao, 15 walikufa na walio hai walikuwa 134 ambao walikuwa wamefichwa kwenye mifuko hiyo.
Seleman alisema wakati wanafanyiwa upekuzi ndipo walipogundua kuna vitu
ambavyo vinafanana na nyoka na kuamua kuwashirikisha wataalamu wa
maliasili ambao walibaini kuwa begi hilo lilikuwa na Kenge.
No comments:
Post a Comment