MBUNIFU wa mavazi na
mtangazaji Bongo, Jokate Mwegelo amesababisha shosti yake, Wema Sepetu
‘Madam’ afurahi baada ya kumpelekea zawadi ya kandambili zake za Kidoti
pamoja na vipodozi mbalimbali.Jokate alisema Wema ni miongoni mwa watu
ambao anawakubali kutokana na mchango mkubwa katika tasnia ya filamu
Bongo, hivyo ameamua kumpelekea zawadi ya bidhaa zake za Kidoti
kuonesha heshima yake.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ akipozi. “Zawadi zangu niliwapa watu mbalimbali mmoja wapo akiwa ni shoga yangu wa kitambo Wema, hii inaonyesha ni jinsi gani nina mapenzi makubwa kwake,” alisema Jokate.
Kwa upande wake Wema, alifurahi na kusema amependa zawadi hiyo anamuomba Mungu azidi kumfungulia milango Jokate katika bidhaa zake mbalimbali anazosa-mbaza.
No comments:
Post a Comment