Inaaminika Cristiano Ronaldo amethibitisha kuachana na Irina Shayk
SIRI imefichuka!. Cristiano
Ronaldo alisherehekea mwaka mpya peke yake baada ya mchumba wake, Mrusi
kutokwenda katika sherehe ya siri aliyoandaa nyumbani kwao Madeira,
gazeti maarufu la Ureno la Correio da Manha rimeripoti.
Gazeti hilo limetoa habari jana
na kuthibitisha kuwa familia ya Ronaldo imevunjika baada kukosekana kwa
maelewano baina ya Ronaldo na mpenzi wake Irina.
Irina mwenye miaka 29 alituma
ujumbe kuwa amejiondoa katika wafuasi wa Ronaldo katika mtandao wa Twite
ambaye ni mpenzi wake wa miaka mitano.
Drama hiyo ilianza baada ya Irina kushindwa kuhudhuria sherehe za tuzo za Ballon d’Or mjini Zurich siku ya jumatatu.
Cristiano mwenye miaka 29
aliungana na mtoto wake wa kiume mwenye miaka minne, Cristiano Jr
jukwaani baada ya kupewa tuzo yake ya tatu ya mwanasoka bora wa dunia.
Katika hotuba yake aliishukuru familia yake, wachezaji wenzake na mashabiki wake, lakini hakumtaja mchumba wake Irina.
Ronaldo na Irina mwaka 2011
Baadaye ripoti zilieleza kuwa
mshambuliaji huyo wa Real Madrid amevunja mahusiano na mwanamitindo huyo
wa Urusi baada ya kugoma kuacha kazi yake na kuwa mke na mama wa
nyumbani.
Vyanzo vya karibu na mwanasoka
huyo wa Ureno vimelieleza gazeti la Ureno la Correio da Manha kuwa
mgogoro huo ulianzia kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mama yake Ronaldo,
Dolere wakati wapenzi hao walipokuwa katika mapumziko ya Krismas mjini
Dubai.
Vyanzo vilisema: “Cristiano
alitaka kumfanyia mama yake ‘sapraizi na alifurahia krismas na Irina
huko Dubai, alipanga kuwa naye katika sherehe ya kuzaliwa ya mama yake,
lakini Irina hakutaka kwenda”.
“Suala hilo lilileta mgogoro
mkubwa na kusababisha kila mtu kufurahia sherehe za mwaka mpya peke yake
na hawajawa na mahusiano mazuri miezi michache iliyopita”.
Gazeti hilo pia limedai kuwa
Irina aliamua kukaa hotelini kwenye moja ya ziara zake Madrid kwasababu
Doleres alipigwa picha akitoa machozi akiwa katika nyumba ya kifahari ya
Ronaldo huko VIP estate La Finca kufuatia mwanaye kushinda tuzo ya tatu
ya Ballon d’Or.
“Dolores anaamini Irina hakuwa mwanamke sahihi kwa mtoto wa Ronaldo,” vyanzo vililiambia gazeti la Correio da Manha.
Irina na Cristiano, ambao
walianza mahusiano baada ya kukutana Armani Photoshoot hawajathibitisha
taarifa hizo rasmi za kuachana.
Msemaji wa Irina amedai kuwa mwanamitindo huyo alishindwa kuhu
No comments:
Post a Comment