Hatimaye nyota ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe Mbwana Samatta imeanza kung’ara katika anga ya kimataifa ya soka.
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba mshambuliaji huyo yupo kwenye majaribio katika klabu ya CSKA Moscow – moja ya klabu kubwa kabisa nchini Urusi ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikitawala soka la nchi hiyo na kucheza katika michuano ya mabingwa wa ulaya.
Samatta alipewa nafasi ya kufanya majaribio ya siku 3 na klabu hiyo kwenye kambi yao ya mazoezi iliyopo Spain, lakini sasa ameongezewa wiki moja ya ziada ili maofisa ya jopo ya ufundi la timu hiyo wapate muda wa kumuangalia vizuri.
Katika moja ya mechi za majaribio alizoichezea CSKA – Mbwana tayari amefunga magoli mawili.
Pamoja na CSKA Moscow – timu nyingine ambazo zinatajwa kumtaka mshambuliaji huyo ni Inter Milan na Udinese za Italia, Atletico Madrid ya Spain, FC Basel ya Uswis na Kaiserslauten ya Ujerumani.
No comments:
Post a Comment