Frank Kalamu akiombewa kanisani.
MAAJABU! Ndivyo unavyoweza kusema unapokutana na mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Frank Kalamu (53) mkazi wa Ilala Jijini Dar es Salaam, aliyetoa ushuhuda wa kufunga mwaka kwamba kwa zaidi ya miaka miwili, alikuwa akipata siku zake kama ilivyo kwa wanawake, ingawa yeye ni kupitia njia ya haja kubwa.
Akitoa ushuhuda huo ndani ya Kanisa la The Revelation lililopo Buza-Kipera Desemba 21 mwaka huu, Frank alidai amepata mateso hayo kwa muda mrefu hukuakizunguka kwa waganga na madaktari wengi bila mafanikio, mbaya zaidi, kwa kipindi chote hicho ameshindwa kushiriki tendo la ndoa na mkewe.
Akizungumza na waandishi wetu nje ya kanisa, Frank alisema awali alikuwa mzima lakini ghafla alianza kwa kukosa hamu ya kushiriki tendo na mkewe, ingawa alipojaribu kuchepuka, alimudu vyema kazi hiyo.
“Baadaye dalili zilizidi kuongezeka, nikajikuta nikipata maumivu chini ya kitovu na kuanza kutoka damu kila mwezi hasa nikiwa najisaidia haja kubwa, hali hiyo huambatana na kutoka nyama sehemu za haja kubwa.

No comments:
Post a Comment