19 December 2014
Huyu ndo mchumba mpya wa Johari wa Bongo Muvi...BAADA YA KUTEMENA NA RAY KIGOSI
MAPENZINI: Swala la mapenzi ni jambo binafsi, lakini linapokuja kwa watu mastaa huwa lazima lilete stori.Leo nimetua kwa mwigizaji nguli na mahili wa filamu hapa Bongo, Blandina Chagula “JOHARI”.
Ni muda mrefu sasa tangu aachane na aliekuwa mpenzi wake wa siri Vicent Kigosi “Ray” ambae pia ni mwigizaji na muongozaji wa filamu, mwana dada Johari kwa mara ya pili sasa ametokelezea akiwa na jamaa mwingine ambae amezua maswali mengi bila majibu kutoka kwa Johari mwenye.
KIVIPI?
Takribani miezi kadhaa iliyopita Johari kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa instagram, aliweka picha hio hapo juu na kuandika “Washa Movie iendelee” kwa wapenzi wa habari za UBUYU hapa mtakuwa mlimsoma vyema dada yetu. Hii ilizua mjadala miongoni mwa mashabiki wake huku wengine wakisema huyu jamaa ndio kachukua nafasi ya kaka yetu Ray wakati wengine wakisema anafanya hivyo ili kumrusha roho Ray ambae kwa wakati huo penzi lake na Chuchu Hans ilikuwa jipya na motomoto. Mbali na comment nyingi kumtaka Johari afunguke, bado Johari alipiga kimya. Mzee wa Ubuyu namimi nikawa kama vile nimeipotezea movie hii.
Kilichokuja na kunifanya niikumbuke movie ni hivi majuzi kuweka picha tena akiwa na jamaa huyo wakiwa kwenye sherehe ya harusi na bila kuandika chochote, kwamaana nyingine aliwachia mashabiki wajiongeze wenyewe...sasa comment zaidi ya asilimia 70 zilikuwa zisomeka, Shemejiiii, mnaendanaaa mara ooh...safi sana.....Ilimradi kila mtu aliandika kile nachojisikia, Johari hakujibu kitu ila wengi waliamni kuwa hapa kuna jamboo na watu kuwa wapo penzini.
Namimi mzee wa ubuyu nikaonasiombaya nikuletee hii movie ili nawe uone na uiache iendelee.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment