17 November 2014
WOLPER AWABWATUKIA WANAOMSEMA
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper.
STAA wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amewabwatukia baadhi ya watu wanaomsema kuwa kafulia na kudai hawajitambui na wanapenda kuzungumza vitu ambavyo hawana uhakika navyo.
Akizungumza na mwandishi wetu, Wolper alisema anashangazwa na watu ambao wanaojifanya ni watabiri wa maisha yake wakati hakuna hata mmoja ambaye anajua ni wapi alipotokea, wanamzushia na kumuandika mitandaoni.
“Jamani kuna watu ambao wanajifanya ni watabiri katika maisha ya watu na ni vyema kila mtu akafuata mambo yake na kuangalia zaidi vya kwao na siyo kunifuatilia leo nimefulia au leo niko sawa, wanaboa sana,” alisema Wolper pasipo kuwataja majina.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Comments system
Disqus Shortname
No comments:
Post a Comment