Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper akishoo love na Wema Sepetu.
UNAFIKI 100%! Wakati kila mtu akiamini kwamba staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ni shosti wa Kajala Masanja ‘Kay’, ameibua mshangao baada ya kunaswa akikumbatiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye kwa sasa haziivi na Kay.
Tukio hilo lililoibua maswali mengi yasiyokuwa na majibu ya harakaharaka lilijiri hivi karibuni katika bethidei ya shosti wa damu wa Wema, Aunty Ezekiel Grayson ambayo ilifanyika kwenye Mgahawa wa Rodizio, Masaki jijini Dar.
WAKUMBATIANA
Huku paparazi wetu akishuhudia na kuwafotoa picha, Wema alipoingia tu ukumbini humo, alimkuta Wolper akila raha zake ambapo alimkimbilia kisha akamkumbatia kwa dakika kadhaa huku wakimwagiana mabusu kuonesha wamemaliza tofauti zao na kwamba walikuwa ‘wamemisiana’.
Wakati wamekumbatiana na kupigana mabusu walikuwa wakinong’onezana mambo yao ambapo walipomaliza waliachia vicheko vilivyosikika ukumbi mzima ndipo minong’ono ikaanza.
Kitendo cha Wema kutumia dakika kadhaa kukumbatiana na Wolper, kilitafsiriwa na wataalam au wafuatiliaji wa mambo ya watu (ubuyu) kuwa ni usaliti mzito kwani Wolper ni Timu Kajala ambaye ni hasimu mkubwa wa Wema.SOMA ZAIDI>>.
No comments:
Post a Comment