WAKATI suala la kudaiwa kudanganya umri likiwa bado ‘bichii’, taarifa zinadai kuwa mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu ametoweka na hajulikani alipo, Risasi Mchanganyiko limechimbua stori kamili.
Mapaparazi wetu walipofika katika nyumba waliyoelekezwa, walikuta imebadilishwa na kuwa Ofisi ya Vikoba ambapo mmoja wa wahudumu wa ofisi hiyo kwa sharti la kutoanika jina lake gazetini, aliwataka waandishi wetu kwenda Mbezi-Makonde akidai ndiko anakoishi kwa sasa.
“Hapa ilikuwa nyumba ya zamani lakini kwa sasa ni ofisi na Sitti hakai hapa, kama mnamtaka nendeni Mbezi-Makonde huko nasikia ndiko anakoishi,” alisema mtumishi huyo.
No comments:
Post a Comment