14 November 2014

MREMBO ANUSURIKA KUUAWA NA DEREVA WA BODABODA!

Mrembo (jina halikufahamika mara moja) aliyenusurika kifo baada ya kugongwa na mwendesha bodaboda aliyefahamika kwa jina moja la Fikiri.
Katika tukio hilo lililotokea hivi karibuni, dereva huyo wa bodaboda akiwa anatokea upande wa Kwamtogole kuelekea Magomeni-Makanya, alipokaribia kona ya kuelekea Magomeni-Kagera ndipo akamvaa mwanamke huyo aliyekuwa akijipitia zake na kumfanya apoteze fahamu kwa dakika kadhaa.DEREVA wa bodaboda aliyefahamika kwa jina moja la Fikiri, nusura amuue mrembo mmoja mkazi wa Tandale-Kwatumbo, jijini Dar baada ya kumparamia na bodaboda kando ya barabara. 

Raia wakishuhudia ajali iliyotokea. Chanzo kimeeleza kuwa, mwendesha bodaboda huyo alikuwa kasi ‘akamu-overtake’ mwenzake lakini baada ya kuchomoza mbele yake alikutana na bodaboda nyingine ambayo alivaana nayo na kwenda kumkumba mrembo huyo, akaanguka na kuzimia.INAENDELEA>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname