14 November 2014

DIAMOND, ZARI GUMZO AIRPORT

Mrembo mkali kutoka Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady (mwenye gauni jekundu) akishuka kutoka gari la ‘Diamond Platnumz’.

BAADA ya kula bata za kutosha Bongo, wakati wakisindikizana kimahaba, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mrembo mkali kutoka Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, wamezua gumzo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, Ijumaa lina mchapo kamili.Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri mishale ya mchana, Jumanne iliyopita katika maegesho ya airport (uwanja wa ndege) ambapo Diamond alikuwa akimsindikiza Zari aliyekuwa akitimua Bongo baada ya kufanya yao kwa siku kadhaa.

Awali kabla ya tukio hilo, gazeti hili lilipokea ‘ubuyu’ kutoka kwa chanzo chake cha kuaminika kwamba, wawili hao walikuwa wakijiandaa katika hoteli waliyokuwa kwa siku kadhaa iliyopo kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi, tayari kuelekea uwanja wa ndege.

Zari au The Boss Lady akimwelekeza kitu mpambe wa 'Diomond'.
“Ijumaa acheni kulaza damu, kwa taarifa yenu Diamond ndiyo anajiandaa kumpeleka Zari airport wahini pale mpate tukio kamili ili kumaliza ubishi kuwa kweli walikuwa wote Bongo,” kilisema chanzo hicho kikiomba hifadhi ya jina gazetini.SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname