MTOTO Omar Mayunga (10) (pichani) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Sombetini jijini hapa, ameshindwa kuendelea na masomo kutokana na ugonjwa wa kuvimba macho na anahitaji msaada wa kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Kilimanjaro, Christian Medical Centre ‘KCMC’.Mtoto Omar Mayunga akiwa na mama yake. Mayunga anayeishi Sombetini na mama yake, alizaliwa na ulemavu wa mdomo na macho bila kujulikana chanzo ambapo katikati ya mwaka huu alijitokeza mfadhili aliyemsaidia kufanyiwa upasuaji wa mdomo uliokuwa umechanika pande mbili kwa kujazwa nyama kisha kushonwa. Akizungumzia ulemevu huo, mama mzazi wa mtoto huyo, Jafara Hussein ambaye ndiye anayezunguka naye mitaani kuomba msaada, alisema mwanaye alizaliwa akiwa na ulemavu huo na kwamba hadi kufikia umri huo ameshindwa kumtibu kutokana na kukosa fedha na muda wote macho huonekana kuvimba na kutiririka machozi.
No comments:
Post a Comment