17 September 2014

WEMA AJIWEKA KANDO MGOGORO BONGO MOVIE

 

Staa asiyekauka kwenye vyombo vya habari Bongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’

STAA ASIYEKAUKA KWENYE VYOMBO VYA HABARI BONGO, WEMA SEPETU ‘BEAUTIFUL ONYINYE’ AMESEMA KUWA, HAWEZI KUJISHUGHULISHA KAMWE NA MGOGORO ULILIPO KWENYE KLABU YA BONGO MOVIE UNITY UNAOMTAKA MWENYEKITI WAO, STEVE MENGERE ‘STEVE NYERERE’ AJIUZURU

Wema alifunguka alipokuwa akijibu swali lililomtaka aeleze mtazamo wake juu ya mgogoro huo ambapo alisema anatambua kwamba hali si shwari klabuni hapo huku baadhi ya wasanii wakidai mwenyekiti wao anachakachua fedha za chama lakini kwa upande wake hataki kujiingiza na ishu na hiyo.
“Mh! Sio rahisi kabisa mimi kuingilia sekeseke hilo kusema eti Steve anafaa kuendelea na madaraka au kuachia ngazi, sitaki kuingilia hilo kabisa maana huwa sifatiliagi sana mambo ya Bongo Movie zaidi ya vitu muhimu tu,” alisema

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname