Mshambuliaji
Mario Balotelli mwenye umri wa miaka 24, aliyehamia Anfield kutoka AC
Milan kwa Pauni milioni 16 mwezi uliopita, jana alitolewa nje katika
mchezo wa kirafiki dhidi ya Wolves baada ya kuzozana na refa, Chris Foy.
Kolo Toure (kushoto) akimzuia Balotelli asiendelee na mzozo
Bahati nzuri, alizuiwa na mchezaji mwenzake, Kolo Toure wakati Foy akizungumza naye kwenye mchezo huo. Chanzo
cha mzozo huo ni baada ya Mtaliano huyo kugongana na mchezaji wa
Wolves. Baada ya mzozo huo tu, Balotelli alitolewa nje mara moja.
Balotelli akielekea nje baada ya mzozo huo
No comments:
Post a Comment