Hivi
ni vitu ambavyo inabidi tu tuwaachie Diamond na Wema waendelee kufanya
yao, wengine wabaki watazamaji tu, afterall siyo kila mtu yuko kwenye
movie yao ambayo bado inaendelea, hii ni moja ya celebrity couple
inayopendwa na watu wengi zaidi nchini Tzee na nje, ila kwa haya
wayafanyayo, hutakuja kuona couple wowote hapa tzee wakifanya haya
wanaofanya yao, labda huko nchi za wengine ila kwa hapa Bongo, ni Wema
Sepetu tu na Diamond Platnumz ndio wanayoweza.
Kudai kutengeneza movie ambayo haijatoka hadi leo”Temptation”Kati
ya vitu ambavyo si rahisi cople wengi kukuta wanafanya pamoja ni movie,
ila kwa hili la wapendanao hawa ni noma zaidi, ndio moja ya celebrity
couples ambao wamewahi kudai kucheza movie wakati walipokuwa wameachana,
ili tu wawe karibu pamoja, ikiwa inasemekanailikwenda kufanyiwa
shooting nchini China, na ikiwa nimwaka wapili huu sasa wamesharudiana,
na movie hiyo haijakamilika bado,huku ikibakia msemo tu “Acha movie
iendelee”.
Hawa ni
moja ya celebririres waliowahi kutangaza kuachana mara kadhaa na mwisho
wa siku kurudiana na hadi hii leo bado wapo pamoja,imetokea kusikia watu
wegi maarufu hapa bongo wakiachana na kila mtu akishia kushika mahesabu
yake, ila kwa Diamond na Wema, ni moja ya couple maarufu zilizowahi
kuachana na kurudiana mara nyingi kuliko mtu yeyote maarufu hapa Bongo.
Unakumbuka yale ya Rihanna kushushiwa kipigo na Chris Brown na bado
akamrudia ?
Wema kumvalisha Diamond wigi na kupost picha mitadaoni.
Kama ni
vituko basi hapa huwa haviishi, saa zingine unaweza kusema ni mapenzi
kuzidi, ila kwa Diamond kuvalishwa wigi, kupigwa picha na mpenzie(Wema)
na kupost kwenye mitandao ya kijamii, Only Diamond na Wema ndio kweli
wanaweza kufanya hivi, katika miaka hata ya baadae, sidhani kama
watatokea couple maarufu wenye vituko kama hivi, ni nadra sana ukute mtu
maarufu wakiume kuvaa wigi la kike, kupiga picha na kupost kwenye
mitandao.
Kurekodi video wakiwa kitandani na kupost kwa mashabiki kuangalia.
Kama ni
love ku-show love kwa mashabiki iko poa zaidi, kwa Diamond na Wema ndio
inasemekana kuwa hata baada ya kudai hapo awali kuwa kwa sasa wanataka
kuweka mambo yao yawe yao binafsi, ila ndio couple waliowazi zaidi
ku-show mambo yao hadharani, si couple wote hapa bongo wenye uwezo wa
kufanya hivi, zaidi ya kujipiga picha wakiwa kitandani na kupost kwenye
media. Tumezoea kuona watu wengi hasa maarufu wakifanya mambo yao kwa
siri zaidi, ila kwa couple hawa wako wazi sana wakifanya mambo yao.
credit : vibe
No comments:
Post a Comment