Ukweli
haufichiki daima labda kuuchelewesha tu! Ndicho kinachomkuta muigizaji
wa kike wa filamu ya ‘Django Unchained’ wa Marekani, Daniele Watts
aliyewapa wakati mgumu polisi wa Los Angeles kwa kuwatuhumu kumnyanyasa
na kumfanyia ubaguzi wa rangi alipokuwa na mpenzi wake Brian James.
Lakini
TMZ wamepata picha na ushahidi kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo ambaye
ameeleza kuwa aliwaona Daniele na mpenzi wake Brian wakiwa katika
harakati za kufanya mapenzi kwenye gari.
Picha
hizo zilizochukuliwa katika eneo la tukio siku ya Alhamisi
zinaomuonesha Daniele na Brian wakiwa wameegesha gari, mlango mmoja
ukiwa wazi wakifanya kilichokatazwa kisheria.
Inaelezwa kuwa mtu mmoja aliyeliona tukio hilo aliwaita polisi na kila kitu kiliwekwa wazi muda huo. Katika sauti iliyonaswa na TMZ, muigizaji huyo anasikika akiwasumbua polisi hao kwa maneno na kutumia 'F-Word' kwenye sentensi zake.
Katika
sauti nyingine iliyonaswa na Mail Online, Daniele anasikika akimwambia
polisi aliyemfunga pingu kuwa anajua haki zake kutokana na uzoefu
alioupata katika uigizaji.
Daniele Watts alicheza uhusika wa poliso katika comedy ya ‘Weeds’ ya mwaka 2012
No comments:
Post a Comment