Msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja akiwa na mumewe mahakamani.
Licha
ya mkwanja kumtembelea, msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja amekwama
kupata pesa ya kumlipia faini mumewe Faraji Chambo ili aweze kutoka
jela.Akizungumzia ombi la mumewe huyo kumtaka kutofuja pesa
badala yake amlipie faini ili aondokane na mateso ya gerezani, Kajala
alisema ni kweli anampenda sana mumewe na angetamani kufanya hivyo
lakini kiasi cha shilingi milioni 200 kinachotakiwa si kidogo hivyo
hawezi kukipata.
“Nampenda
sana mume wangu, hilo halina ubishi na pia najua anateseka sana kule
gerezani kwani nakujua lakini milioni 200 siyo hela ndogo ujue.
“Natamani hata leo niwe nayo nimlipie lakini ndiyo hivyo tena,” alisema
Kajala kwa masikitiko.
Hata
hivyo, licha ya Kajala kuwa na nia ya kumtoa jela mumewe, mmoja wa
mawakili aliyekuwa akihusika na kesi yao aliyeomba hifadhi ya jina lake
alisema:
“Kama
Kajala anafikiria kumlipia mumewe faini simshauri afanye hivyo kwani
hukumu iliyotolewa ni ya kesi moja na ile nyingine ya kuuza nyumba
iliyokuwa imewekwa bondi na Takukuru, bado inaendelea na huwa Faraji
anatoka gerezani kwenda mahakamani.
“Sasa
Kajala anaweza kutoa pesa zake, mumewe akatoka lakini hukumu ya ile kesi
nyingine ikatolewa na akarudi tena jela,” alisema wakili huyo. Hivi
karibuni, mume wa Kajala alituma ujumbe kupitia watu wanaokwenda
kumtembelea akimtaka mkewe kumuonea huruma na kumlipia faini ili atoke
gerezani badala ya kuzitumia pesa kwa anasa.
No comments:
Post a Comment