KIJANA ANASWA LAIVU KWA KUUNDA MTAMBO WA KUWAIBIA AZAM, ZUKU.
Bw.
Ali anayedaiwa kuunganisha visivyo halali, mitambo ya kurusha matangazo
ya televisheni ya vituo mbalimbali kwa malipo rahisi.
Katika hali
ya kushangaza, mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Ali, mkazi wa
Mwananyamala jijini Dar, amekamatwa na polisi baada ya kudaiwa
kuunganisha visivyo halali, mitambo ambayo iliwawezesha watu kuangalia
matangazo ya televisheni ya vituo mbalimbali kwa malipo rahisi.
Awali,
msamaria mwema mmoja alipiga simu kwa kikosi kazi cha Operesheni Fichua
Maovu (OFM) cha Global Publishers na kukitonya juu ya uwezo wa mtu huyo
anayewashangaza kwa utaalamu wake wa kuunganisha mitambo hiyo bila
kugundulika.
Baadhi
ya ving'amuzi vilivyokuwa vikitumiwa na mtuhumiwa kuunda mtambo wa
mawasiliano. “Hapa kuna watu kama 80 hivi wameunganishwa, wanaangalia
televisheni za Azam, Zuku na nyingine kwa bei chee, lakini wanaangalia
mipira, filamu na kila kitu, yaani huwezi kuamini kaka,” chanzo hicho
kilinyetisha kwa OFM.
Bw.
Ali (kushoto) akibanwa kwa maswali juu ya biashara haramu anayofanya.
Katika kujiridhisha, kikosi kazi chini ya kamanda mkuu, kilitembelea
eneo la tukio na kufanya ukaguzi wa siri, uliothibitisha kuwepo kwa
huduma hiyo, lakini bila ya kuwepo kwa dekoda za vituo hivyo vya
televisheni vinavyotolewa kwa malipo.
Ulinzi
mkali ukiimarishwa nje ya nyumba ya Bw. Ali. Baada ya kujiridhisha
huko, OFM ilifanya mawasiliano na wahusika wa vituo hivyo, ambao nao
walitembelea eneo hilo la tukio na kujionea wenyewe. Wahusika hao
walikuwa ni Afisa Leseni wa DSTV na Afisa Mauzo wa Azam Tv pamoja na mtu
mmoja kutoka chama cha hakimiliki cha COSOTA.
Afisa
Leseni kutoka chama cha hakimiliki COSOTA, Zephania Lyamuya (kulia)
akisimamia zoezi. OFM iliwashauri maofisa hao kuripoti jambo hilo kituo
cha polisi, ushauri ambao waliukubali na kwenda kutoa taarifa Kituo cha
Polisi Oystebay ambao waliongozana na watu hao hadi Mwananyamala.
Madishi
ya Satelaiti yanayotumiwa na Bw. Ali kurushia matangazo ya televishen
yakiwa juu ya nyumba yake. Kufika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo ambaye pia
ni maarufu kwa jina la utani kama Masetelaiti, Polisi walifanikiwa
kumkamata na baada ya upekuzi, waligundua kuwepo kwa mitambo ya aina
mbalimbali, vikiwemo ving’amuzi vya aina mbalimbali, modulators,
Receivers na vifaa vingine vikionekana vikiwa vimeunganishwa kwa
utaalamu wa hali ya juu katika ukuta wa sebule yake.
Afisa
Mkuu wa Mauzo kutoka kampuni ya Azam, Shah Seffu akiwa nje ya ofisi ya
Bw. Ali. Masetelaiti alikiri kuendesha maisha kwa staili hiyo na kudai
kuwa utaalamu wa kuunganisha ving’amuzi hivyo ni wake mwenyewe na
amekuwa akifanya hivyo kwa muda mrefu.Afisa Leseni kutoka Cosota,
Zephania Lyamuya alisema jamaa huyo anastahili kupelekwa Polisi kutoa
maelezo kwani licha ya kutokuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo, pia
amekuwa akiwanyonya waigizaji wanaostahili kulipwa kila filamu zao
zinaporushwa katika televisheni za nje.
Kikosi
kazi kikifungua mitambo na kuharibu kazi haramu ya Bw. Ali. Naye Afisa
Mkuu wa Mauzo kutoka kampuni ya Azam aliyejitambulisha kwa jina la Shah
Seffu (pichani kulia), alisema kuwa operesheni hiyo ni moja kati ya
hatua walizozipanga kumaliza tatizo la kuingilia mawasiliano ya
televisheni jambo ambalo limeonekana kukua kwa kasi nchini.
Baadhi
ya Ving'amuzi vilivyokusanywa kutoka katika mtambo uliosukwa na
Masatelaiti. Baada ya kuvikusanya vifaa hivyo vilipelekwa katika Kituo
cha Polisi cha Oysterbay sambamba na mtuhumiwa kutoa maelezo ambapo
jalada lilifunguliwa
No comments:
Post a Comment