MTANGAZAJI wa Kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa kupitia Radio Clouds FM ya jijini Dar, Loveness Malinzi ‘Diva’ kwa mara ya kwanza, amejilipua kuzungumzia uhusiano wake na Zitto Kabwe kwamba walikuwa mke na mume.Katika
mahojiano maalum na mwanahabari wetu jijini Dar juzi, Diva alisema
anashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari (siyo vya Global Publishers)
kumnyima uhuru wa kuongelea suala lake na ‘zilipendwa’ wake huyo wakati
kisheria yeye ni mke wake hivyo anapaswa kuzungumzia kutengana kwao.
“Ninyi mnayaongelea mambo ya Zitto
na mimi juu kwa juu tu hamjui kama mimi nimeishi naye kama mke na mume
nyumbani kwake Masaki (Dar), sasa nini
kilisababisha penzi letu kuvunjika watu hawajui, nina ushahidi wa
kutosha lakini wanaongeaongea tu,” alisema Diva.Akaongeza: “Sasa
ninavyojua mimi kwa sheria za nchi, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja
kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mke na mume. Hawezi kuniacha
kirahisirahisi tu.

No comments:
Post a Comment