Aliekuwemo
kwenye hili basi ndio amenitumia hizi picha na kuniambia watu wasiozidi
watano wamefariki dunia wengine zaidi kujeruhiwa baada ya basi lao
kuanguka Mkange Berega.Basi linaitwa Air Bus na limepata ajali
likielekea Dodoma kutokea Morogo na ni baada ya kifaa cha usukani
kushindwa kufanya kazi ambapo muda mfupi baadae anasema alisikia tu
dereva akipiga kelele na kisha kikafata kishindo, basi likaacha njia na
kwenda bondeni.jali hii imetokea siku tatu baada ya Waziri wa uchukuzi
Dr. Harryson Mwakyembe kufungia kampuni mbili za mabasi ya J4 Express na
Mwanza Coach yaliyogongana na kuua 39 Musoma.
U
No comments:
Post a Comment