Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Cecilia Hamis (pichani), mkazi wa Majoe Mjimpya Relini jijini Dar es Salaam amemlalamikia mumewe aliyemtaja kwa jina la Hamis Juma kwamba ametembea na mbwa wao mweusi hadi kumpa mimba.
Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake, mwanamke huyo alisema alibaini hilo wiki mbili zilizopita.
“Nililigundua hilo wiki mbili zilizopita. Nakumbuka ilikuwa usiku nikiwa nimelala, nikamsikia mbwa mmoja (kati ya wawili) analia. Niliamka kwenda kuangalia ili kujua sababu, kufika nikawasha tochi ya simu, nilishangaa sana kumwona mume wangu yuko naye anafanya mapenzi.
“Nilimuuliza anachokifanya, akasema anammalizia shida zake kwa kuwa hakuna mbwa wa kiume wa kumsaidia,” alisema mwanamke huyo.
Akiendelea kumlalamikia mume wake kwa madai hayo mazito, mama huyo alisema:
“Siku iliyofuata usiku tena, nikiwa nimelala nilimsikia mbwa akilia, nikaamka. Safari hii niliambatana na watoto wangu, tukaenda nje, kufika tukamshuhudia mume wangu akifanya tukio kama la jana yake, nilipomuuliza akanipa majibu yaleyale kwamba anammaliza shida zake mbwa huyo.” Akaendelea: “Hawa mbwa waliletwa wawili wakiwa wadogo kabisa na wote ni majike na tangu walipoletwa sijawahi kumwona mbwa dume hata siku moja kwani mara nyingi tunawafungia kwenye banda lao.
“Na tangu mume wangu aanze mchezo huo huyo mbwa mmoja mweusi (pichani) amenawiri kupita kiasi, naamini amempa mimba.”
Mwanamke huyo alisema kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo, aliamua kuwaeleza majirani ambao nao walimshauri aende kuripoti kwa mjumbe wa eneo hilo.
Akizungumza na Uwazi, Mjumbe wa Shina Na. 26, Majoe Mjimpya, Mbaruka Nyamaishwa alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa mwanamke huyo akamshauri kuyapeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Stakishari.
Habari zaidi zinawekwa wazi kwamba, majirani nao walipoona mwanamke huyo anachelewa kwenda polisi, wao walimsomba na kwenda naye ambapo walitoa taarifa katika Dawati la Jinsia.
Mkuu wa dawati hilo, Koplo Golbert aliongozana na walalamikaji hao hadi nyumbani kwa mdaiwa ambapo alimkagua mbwa huyo na kuwaamuru wanandoa hao kuripoti kwenye kituo hicho cha polisi bila kukosa jana Jumatatu saa 3 kuonana na mkuu huyo na uchunguzi kuendelea.
Uwazi lilimuuliza swali moja mwanamke huyo, ni kwa nini anasema aliamka na kutoka nje usiku bila kueleza mumewe anakuwa wapi muda huo kwani hakuonyesha kushangaa kutomwona kitandani?
Anajibu: “Tulitengana vyumba kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia.”
Uwazi lilimgeukia mume wa mwanamke huyo na kumuuliza kuhusu madai mazito ya mkewe ambapo alisema:
“Mimi sijawahi kufanya kitendo hicho na mbwa ila nahisi mke wangu na hawa majirani wa hapa wananitengenezea hilo tukio ili nikafungwe jela maisha, halafu wao waweze kuchukuwa mashamba yangu kwani ndani ya ndoa yangu kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara.”
Uwazi lilitilia shaka uwezekano wa mbwa kunasa mimba ya binadamu, hivyo lilimsaka daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kumuuliza kuhusu madai ya mwanamke huyo.
Msikie: “Mh! Binadamu kumpa mimba mbwa haiwezekani. Binadamu anaweza kumpa mimba sokwe, kwa mbali sana nyani. Lakini si mbwa.
“Ila kama huyo mama anasema hivyo, mbwa akapimwe na ikibainika ni kweli basi yatakuwa maajabu ya dunia maana dunia ina mambo yake.”
No comments:
Post a Comment