24 August 2014

HUYU NDO MTOTO WA MBUNGE WA TEMEKE ALIYE SHINDA TAJI LA MISS TEMEKE

Shindano la kumtafuta mrembo wa Temeke, Miss Temeke 2014 yalifanyika jana usiku katika ukumbi wa TCC Chang’ombe, jijini Dar es Salaam ambapo Sitti Mtemvu aliibuka mshindi.

Sitti Mtemvu, Miss Temeke 2014
Sitti Mtemvu alilivaa taji hilo na kuwa mshindi wa kwanza huku mrembo Salama Saleh akishika nafasi pili, na Neema Mollely alitajwa kuwa mshindi wa tatu.
Matokeo hayo yanawapa warembo hao watatu  tiketi ya kuwa wawakilishi wa Wilaya ya Temeke katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania 2014).

Shindano hilo lililokuwa na washiriki 17 lilishereheshwa na Gardener G. Habash, mtangazaji wa kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm lilipambwa na burudani toka kwa wasanii mbalimbali akiwemo TID na Young Suma.


Gardener G Habash akiwa na Abdalah Gunda wa kitengo cha masoko cha Airtel
Meza ya Majaji

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname