1. Ukienda kwake ukutane na vyombo vichafu na nguo chafu zimejazana usidhani ni mvivu, ni kamtihani anakupa.
2.
Ukiingia kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi anayekujaga
mara moja kwa wiki aje afanye usafi alipwe usidhani eti anajali kihivyo.
Anakutest aone kama utasema "Acha baby, ntakufulia mpenzi wangu".
3.
Ukikuta kwake amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama unga,
mchele, na vingine halafu akakwambia mwende ule mgahawa fulani mkapate
dinner usidhani eti ana hela kibao ya kutumia! Anakutest aone kama
utamwambia mbaki kwake mpike mle. Uko chumba cha mtihani!
4. Siku
kakuahidi kukutoa out halafu unafika kwake unakuta kajikunyata kama
mgonjwa anakwambia mama ake kapiga simu anaumwa anaomba atumiwe hela.
Halafu anakwambia hela aliyo nayo na ukipiga mahesabu unaona ni kama ile
ya kutumia mkiwa out. Anakuomba ushauri afanyaje. Wewe unamwambia "Baby
twende out, suala la mama nina uhakika kaka zako na dada zako
watalishughulikia, atawapigia". Woiyeeee! My sista hapo umejimaliza!!
5.
Ukimtembelea kwake ukakuta anapika na kufanya usafi wewe Umekaa tu
unaangalia muvi halafu ukitaka umsaidie anakwambia endelea kuangalia
muvi karibu anamaliza na wewe kweli ukarudi ukakaa kuendelea na muvi
yako! Siku zako zinahesabika!!
6. Ulishawahi kumwambia mpenzi
wako aende kwenye ibada? Alipokataa ulimsisitizia? My sister, hata
walevi wanapenda wanawake ambao wanawasisitiza kwenda kwenye ibada. Sio
tule wale kila siku wanashinda baa na club.
7. Mara ngapi huwa
unamkumbusha kuwapigia simu wazazi au ndugu zake kuwajulia hali mkiwa
wote? Angalao akupe na simu na wewe uwasalimie? Huo ni mtihani mwingine
huwa mnafeli sana.
8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza kabla ya
ndoa. Sio kila saa ukimtembelea ni kujiachia tu. Inaleta adabu na
inawafanya mkazanie kufikia lengo kubwa la maisha.
9. Jaribu
ukiwa unaenda kwake uwe unaenda na tuvitu kama nyanya, vitunguu, n.k.
Hivyo vyote huwa wanaume ni shida kununua mara nyingi.
10. Wakati
mwingine nenda kwake hata na CD za dini mpelekee msikilize. Sio kila
ukifika kwake wewe ni rege, Eminem, Lil Wayne na kina nani sijui. Ukiwa
hivyo hataona tofauti kati yako na wale macho juu anakutana nao club
kila wikiendi.
11. Jenga na tabia ya kumnunulia tuzawadi tudogo
tudogo. Sometimes unakuja na boksa au kavesti au kadodoranti. Hiyo kwa
wanaume inaonyesha unaweza kujipa majukumu na kuyasimamia. Marks hizo.
Ila Angalizo����
---Unaweza fanya yote hayo na ukaachwa solembaaa
No comments:
Post a Comment