27 June 2014

NISHA: NIKIPITA MTAANI NAKIMBIZWA



MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka kuwa kuna wakati aliwahi kujikuta katika wakati mgumu baada ya umati wa watoto kumkimbiza mtaani huku wakimwimbia nyimbo baada kumuona kwa mara ya kwanza uchochoroni.

Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’
Akizungumza na paparazi wetu, Nisha alisema tukio bichi lilitokea mwaka jana katika moja ya mitaa ya Zanzibar ambapo ghafla watoto walianza kumkimbiza nyuma na kumtania kwa kuigiza baadhi ya vipande vya filamu alivyoigiza mpaka akakereka.


“Walikuwa wakinikumbushia filamu ambazo nimecheza kama mchekeshaji lakini kuna wakati nikaona imezidi na nilipojaribu kuwakimbia, walinikimbiza huku wakiimba mpaka nikajisikia vibaya,” alisema Nisha.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname