Kwa muda mrefu Wolper amekuwa makini na picha zake za kimahaba tangu alipokuwa akitoka kimapenzi na mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
CHANZO CHAMWAGA MTONYO
Awali, chanzo makini kilipenyeza habari kuwa kuna mawasiliano yamenaswa ‘kimafia’ ambayo yalitoka kwa Wolper kwenda kwa rafiki yake yakionesha anabanjuka na mwanaume huyo wa mtu aliyejulikana kwa jina moja la Gee.
YADAIWA NI MUME WA SHOSTI YAKE
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba licha ya kuwa ni mume wa mtu, mwanaume huyo ni bwana wa rafiki yake kutokana na mawasiliano hayo yalivyosomeka.
“Mashabiki kila siku huwa wanamtetea Wolper na skendo zake, sasa nakutumia picha pamoja na ‘chating’ zake alizokuwa akichati na shoga yake kuhusiana na jamaa huyo,” kilisema chanzo hicho.
PICHA ZATUA RISASI JUMAMOSI
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wa Risasi Jumamosi alimtafuta sosi huyo na kufanikiwa kuzitia kibindoni picha hizo kisha kazi ya kuwasaka wahusika ikaanza.
Wa kwanza kutafutwa alikuwa ni Gee ambaye kwa mujibu wa vyazo tofauti, ilidaiwa kuwa kwa sasa hayupo Bongo na hakuacha mawasiliano yoyote tangu alipoondoka.
WOLPER SASA!
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, paparazi wetu alimtwangia simu Wolper ambaye alieleza kila kitu: Paparazi: Mambo vipi Wolper, nasikia makelele unaweza kusogea sehemu yenye utulivu kuna ishu nataka tuongee?
Wolper: Niko msibani na sasa hivi ndiyo zoezi la kuaga mwili, ngoja niingie kwenye gari nikupigie.
Baada ya dakika 45
Wolper: Haya niambie wangu niko sehemu nzuri. Paparazi: Ni hivi, kuna habari imetufikia ikiambatanishwa na picha na baadhi ya chating inakuhusu wewe! Wolper: Habari gani hiyo mbona unanitisha?
Paparazi: Kuna picha zinakuonesha wewe ukiwa katika pozi la kimalavidavi na jamaa anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu. Ukiachana na picha hizo, zimeambatanishwa chating zinazoonesha ulikuwa ukichati na rafiki yako kumueleza kuwa mwanaume uliye naye ni mume wa mtu!
Wolper: Kiukweli kabisa bila ya hata kupepesa macho hizo picha ni zangu na zimepigwa kwa kutumia simu yangu tangu mwaka juzi lakini kuhusiana na hizo chating siyo zangu hata wewe unaweza kuwa shahidi kwani mara nyingi huwa tunachati na unajua vizuri ‘floo’ yangu katika kuandika SMS.
Paparazi: Ok, sawa, lakini turudi katika suala la picha, huyu ndiyo bwana’ko wa sasa?
Wolper: Hapana, huyo ni mshikaji wangu tu na tulipiga picha hizo tukiwa baa tena kipindi kile nahamia tu Mwananyamala (Dar) na sasa hivi hata sijui huyo mshikaji yuko wapi.
Paparazi: Ina maana huna mawasiliano naye kwa muda mrefu, mtu ambaye mlipiga naye picha kimahaba namna hii?
Wolper: Kweli kabisa, sina mawasiliano naye kitambo nikimaliza tu kuongea na wewe nitamtafuta na kumuuliza kulikoni picha hizo kuvuja.
Paparazi: Si ulisema umepiga katika simu yako wewe si ndiyo wa kujiuliza kwa nini picha zimevuja? Wolper: Nilimzawadia simu kama rafiki yangu na picha zikiwa humohumo sikuzifuta. Paparazi: Haya Wolper ngoja nikuache mi niendelee na majukumu. Wolper: Poa wangu baadaye nitakucheki.
WOLPER HUYUHUYU
Hii ni mara ya pili kwa Wolper kutuhumiwa kukwapua bwana wa rafiki yake. Hivi karibuni mshiriki wa Miss Tanzania 2012, Husna Maulid alilalamika kuwa Wolper kamchukulia bwana’ke aliyemtaja kwa jina moja la Rajab, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Si Wolper pekee, ‘trendi’ inaonesha kuwa mastaa wengi wa kike hasa wa filamu wamefanya ishu ya kuporana wanaume kuwa sehemu ya utamaduni katika tasnia hiyo bila kujua wanajiondolea heshima mbele ya jamii.
No comments:
Post a Comment