Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper akipozi.
Wolper kiimani ni Mkristo lakini hivi
karibuni alibadili na kuwa Muislam kabla ya kurejea tena kwenye imani
yake ya awali ya ukristo.
Akizungumza na Risasi Jumamosi juzikati,
Shehe Salum, alisema Wolper anapaswa kujichunguza na kubadilika haraka
kwani kitendo anachofanya ni kinyume na taratibu za dini.
“Siyo vizuri hata kidogo na hata dini zote zinakemea kitendo cha kuchezeachezea dini kwani ni chukizo kwa Mungu.
Jacqueline Wolper akiwa kazini.
“Kwa upande wa Dini ya Kiislamu, kuna
sheria kali zaidi kwa mtu akionekana na tabia hiyo, anaweza hata kuuawa
hivyo wanaofanya mchezo huo waache kwani siyo vizuri. Huko ni kumfanyia
Mungu dhihaka,” alisema Shehe Salum na kuongeza:
“Unajua suala la imani ni kitu
kinachomhusu mtu binafsi, ni vyema kufanya uamuzi wa hakika na kushika
njia moja na siyo kufanya dhihaka na dini ya Mwenyezi Mungu. Ni kitu
kibaya sana.”
Naye Juma Suleiman, mkazi wa Ilala,
jijini Dar es Salaam alimwambia mwandishi wetu kuwa, katika imani ya
kiislam kunakatazwa watu kucheza na dini huku akisisitiza anayefanya
hivyo anaweza kulaaniwa.
“Dini siyo kitu cha kuchezea, ni daraja
la kumfikisha mtu kwenye haki, si mahala pa kuingia na kutoka, kuingia
na kutoka. Huko ni kucheza na Mungu. Namshauri huyo mtoto (akimaanisha
Wolper) abadilike. Asifanye mchezo na imani, Mungu anaweza kumlaani kwa
kumchezea,” alisema Suleiman.
No comments:
Post a Comment