(April 30), Kampuni ya Weusi ilizindua rasmi video ya
wimbo wao ‘Gere’ pale Mediteraneo Hotel, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
watu wengi maarufu na mashabiki.
Uzinduzi huo ulifunguliwa kwa Live Show toka kwa wasanii waliowahi kushiriki Tusker Project Fame, Hisia na Damian Soul.
Hisia ndiye aliyeanza kufanya Live Show kwa gitaa na kuwapa zawadi
watu waliohudhuria uzinduzi huo kwa kuimba wimbo ambao bado hajaurekodi
unaioitwa ‘Give Me a Call’ na kuwataka watu wampe maoni kama aende
akaurekodi au aachane nao.
“Kaurekodi…ingia studio.” Walisikika watu wakisema kwa sauti ya juu
baada ya kuguswa na uimbaji mzuri wenye mguso wa wimbo huo wenye ujumbe
wa mapenzi aka wimbo wa kitandani.
Ingawa wimbo huo uliimbwa kwa mara ya kwanza, watu waliweza kushika
baadhi ya maneno ya kuitikia kuimba nae wakati anaurudia mara ya pili.
Hisia alifuatiwa na muimbaji wa muziki wa Soul Tanzania, Damian Soul
ambaye aliwafanya watu waliohudhuria kuendelea kushangilia kama
walivyofanya kwa Hisia. Damian aliimba nyimbo tatu, moja alirudia wimbo
wa RnB wa Marekani na kufanya nyimbo zake mbili yaani ‘Ni Penzi’ na
‘Hakuna Matata’.
Baada ya show hizo, watu waliiangalia kwa mara ya kwanza video ya wimbo wa ‘Gere’ iliyoongozwa na Enos Olik nchini Kenya.
Video hiyo iliyotengenezwa kwa ubunifu wa kiafrika, inawaonesha
rappers hao wakiwa katika muonekano wa mavazi ya kiafrika na wamejipaka
rangi kama wanaoenda jando, huku warembo wakionekana pia katika
muonekano huo. Lakini pia video hiyo imechanganywa na muonekano wa
wahusika wakiwa ndani ya mavazi ya vijana wa kisasa.
Mchanganyiko huo na ubora wa hali ya juu wa uchanganyaji picha zenye
muonekano mzuri, unatoa picha kuwa video hiyo inaweza kuonekana kwenye
vituo vikubwa vya TV duniani muda si mrefu.
Ubora na ubunifu uliotumika kwenye video hiyo uliwafanya watu waombe irudiwe tena na tena…na kuoneshwa mara mbili.
Ilikuwa kama siku inaanza upya baada ya Weusi kupanda jukwaani
kufanya ‘ukamilifu’ wa uzinduzi huo ambapo walifanya show nzuri
iliyowafanya watu waliohudhuria kupiga kelele za shangwe mara kwa mara
huku wakiimba kwa sauti pamoja na kundi hilo na kucheza hits kadhaa za
Weusi.
Upendo uliooneshwa na watu waliohudhuria ulikuwa sehemu kubwa ya
furaha ya Weusi ambao mara kwa mara walikuwa wakiwashukuru watu
waliohudhuria na kuwaonesha upendo pia... “We love you guys... It’s too
much. Tunawapenda sana yaani.” Joh Makini.
Baadhi ya watu maarufu waliohudhuria ni pamoja na Profesa Jay, Mwana
Fa, AY, Ommy Dimpoz, Vanessa Mdee, Producer wa ‘Gere’ Nahreel na kundi
lake ‘NavyKenzo’, Watangazaji wa Radio na Television Tanzania.
No comments:
Post a Comment