Wakaazi wa kijiji kimoja
Magharibi mwa Sri Lanka wamesema kuwa wameshangazwa na pia kufurahishwa
na tukio la 'kunyeshewa' na mvua ya Samaki wadogo.
Samaki hawa ambao walikuwa katika hali nzuri ya kuweza kulika wanaaminika kuwa walibebwa kutoka kwa mto kwa upepo mkali.Hili si tukio la kwanza la aina hii kuwahi kutokea Sri Lanka- mwaka wa 2012, kulitokea kisa cha mvua ya viumbe vya baharini vijulikanavyo kama 'Kamba' ambavyo huliwa
Wanasayansi wamesema kuwa mvua ya Samaki hutokea wakati ambapo upepo mkali unazinga juu ya maji ya kina kifupi na hivyo kusababisha mzunguko wa maji unaovuta karibu kila kitu kilicho ndani ya maji ikiwa ni pamoja na samaki na hata Vyura.
Wanakijiji wanasema kuwa mvua hiyo ya Samaki ilinyesha Jumatatu huku viumbe wale wakianguka kwenye mashamba, barabara na paa za kijiji hicho.
Baadhi ya samaki hao wenye urefu wa kati ya sentimita tano na nane, walikuwa bado wako hai na walitiwa kwenye ndoo za maji na wanakijiji waliowatumia kama kitoweo badaye.
Hii ni mara ya tatu kwa tukio kama hili kufanyika Sri Lanka, ingawa katika eneo tofauti.
Kando na ile mvua ya ‘Prawn’ya mwaka wa 2012 kusini mwa Sri Lanka, mvua ya kimondo (meteors) nyekundu na manjano ilinyesha mwaka huo huo,tukio ambalo bado linachunguzwa na wanasayansi wa Marekani na Uingereza.
Samaki wamadhamana kuu Sri Lanka.
No comments:
Post a Comment