Mtoto
mwenye umri wa miaka (14) ambaye ni mwenyeji wa Rombo mkoani
Kilimanjaro anayeripoti manyanyaso kutoka kwa mtu anayedaiwa kuwa bosi
wake.
Mtoto mwenye umri wa miaka (14) anadaiwa kuajiriwa akiwa na umri mdogo kinyume cha sheria za kazi kisha kupokea kipigo na manyanyaso kutoka kwa mtu anayedai ni bosi wake aliyemtaja kwa jina moja la Agness.
Kwa
mujibu wa mashuhuda, mbali na kuwepo kwa malalamiko ya unynyasaji juu
ya mtoto huyo, siku ya tukio mwajiri wake alimpa kipigo kwa madai kwamba
alimuibia shilingi laki saba dukani alikomwajiri maeneo ya
Mwananyamala, Dar hivi karibuni.
Mtoto
huyo ambaye ni mwenyeji wa Rombo mkoani Kilimanjaro alizama jijini Dar
na kuajiriwa katika duka hilo mwanzoni mwa mwezi Novemba, mwajka jana.
Akizungumza
na mwanahabari wetu kwa masikitiko, mtoto huyo alisema tangu aajiriwe
na mama huyo hajawahi kulala nyumbani bali alikuwa akilala hukohuko
kwenye duka ambalo ni dogo halafu limejaa vitu vingi na alikuwa
akifungua saa 12:00 asubuhi na kufunga saa 5:00 usiku kila siku.

No comments:
Post a Comment