25 February 2014

MBUNGE ABOOD AMWAGA MISAADA KWA VIKUNDI VYA VIKOBA NA VIJANA MORO

 Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Aziz Abood akitoa jezi kwa wachezaji wa timu ya  maskani Fc iliopo kata ya Mjimpya mjini hapa.
 Mbunge huyo akisalimia na diwani wa kata ya Mindu Hamis Msasa akiteta jambo na mbunge huyo nje ya ofisi ya mbunge huyo jana.
 Mbunge wa jimbo la Morogoro Aziz Abood akitoa hundi kwa kikundi cha wanawake cha vikoba cha mjini hapa.


 Viongozi wa kikundi cha vikoba cha wanawake polisi cha mjini hapa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea hundi shilingi 300,000 kwaajili ya kutunisha mfuko wao kutoka kwa mbunge wa Morogoro mjini.
 mbunge huyo akitoa hundi kwa kikundi hicho cha wanawake polisi
 kikundi cha wanawake cha kupika cha Mazimbu mjini hapa wakipokea vyombo  vya kufanyika kazi kutoka  kwa mbunge huyo

 Habari zaidi soma hapa
MBUNGE wa jimbo l a Morogoro mjini Abdullazizi Abood ametoa msaada wa fedha na vitu mbalimbali vyenye thamani ya  shilingi milioni  2.53 kwa vikundi vya wanawake nane vilivyopo katika manispaa ya Morogoro ikiwa ni kuelekea siku ya wanawake duniani.
Akitoa hundi ya fedha kwa vikundi hivyo Abood aliwataka wanawake hao kuhakikisha wanatumia msaada huo wa fedha kwa manufaa ya kujikomboa kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
Aidha Abood alisema kuwa kuwapo kwa vikundi vya wanawake katika maeneo mbalimbali nchini kunalenta maendeleo ya dhati na hata wanawake kuthaminiwa na waume zao kutokana na kuongezeka kwa kipato katika familia zao.
“Misaada ninayotoa kwamba nina fedha sana ila najua majukumu waliyonayo wanawake nchini hasa katika jimbo langu kwani nimeweza kufanya ziara jimbo langu lote na kujionea matatizo ya wanawake yanayowakabili,na nia yangu ni kuhakikisha wanajikwamua na umaskini na kuweza kujitegemea wenyewe”alisema.

Mwenyekiti wa kikundi cha Polisi Slab vikoba Ukende Ugula akizungumza kwa niaba ya wenzake alimuomba mbunge huyo kuendelea kutetea haki za wanawake na ,watoto na kuhakikisha masuala ya wanawake yaliyopo katika rasimu ya katiba yanaingizwa katika katiba mpya.

Pia alisema kuwa bado kunatatizo la wanawake wengi hasa wa vijiji kutojua haki zao,na kumtaka mbunge huyo kutokata tamaa ya kusaidia wanawake hasa katika mkoa wa Morogoro.
Vikundi vilivyopatiwa msaada ni Tushikamane,Polisi Slab vikoba,Dirisha la maendeleo kutoka chuo cha maendeleo morogoro,Tujishike,Changamka,Ushindi,Tushikamane bigwa na kikundi cha mapishi cha Modeco kilichopatiwa vifaa vya kupikia na kugawa chakula

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname