20 February 2014

HONEY KAUR MAIR AIBUKA MSHINDI WA SHINDANO LA VALENTINES DAY SPECIAL LILILOANDALIWA NA MeTL KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK

1 (5)
Honey akiwa amepozi pembeni ya kikapu maalum cha wapendanao, kilichosheheni zawadi mbali mbali.
Na.Mwandishi wetu
Honey Kaur Mair, ni msichana mwenye bahati. Bila shaka sikukuu yake ya wapendanao ilimalizika kwa furaha baada ya yeye na mumewe kuibuka kidedea wa shindano lililoandaliwa na kudhaminiwa na METL la Valentines Day Special Competition kupitia ukurasa wao wa Facebook.
Pamoja na kuzawadia kikapu maalum cha wapendanao kilichosheheni zawadi kem kem, pia wapenzi hawa walipatiwa vocha maalum iliyowawezesha kupata dinner matata usiku wa siku ya Wapendanao katika mgahawa maarufu wa AK's Cafe.
1511482_472007099595581_152425816_n
Shindano hilo lililoshika kasi kuanzia tarehe 5 February na kumalizika tarehe 12 February, lilishuhudia washiriki wengi wakijitosa kuwania zawadi maalum iliyoandaliwa kwa kutuma picha za couple zao na wapenzi au watu wao wawapendao ambao wangesherehekea pamoja sikukuu ya wapendanao na picha zao kuwekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa METL kisha kupigiwa kura.
Hatimaye baada ya mchuano mkali, Honey na mpenzi wake Davinder waliibuka kidedea kwa kushinda baada ya picha yao kupata LIKES nyingi kushinda wengine hivyo kumaanisha kwamba wao ndio wamechaguliwa na wengi kama 'best couple' kushinda shindano hilo.
1661983_472006856262272_804463697_n
METL inapenda kuwapongeza Honey na Davinder kwa ushindi huo na pia inawashukuru wateja wake wote ambao walishiriki kwa moyo katika shindano hilo. Kwetu sisi, nyote ni washindi, na hawa ni wawakilishi wenu tu katika kuchukua zawadi!
ASANTENI, ENDELEENI KUPENDANA KILA SIKU!
Like Ukurasa wetu wa Facebook hapa www.facebook.com/MeTLGroup

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname