20 February 2014

ALIYEMPA MIMBA SHILOLE NA KUZAA MTOTO, SASA AMTAKA MWANAE,

Picha ya shilole na makala enzi hizo
KWA mara ya kwanza, mzazi mwenza na msanii wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Elias Makala ameibuka na kujinadi hadharani wilayani Igunga, Tabora.
Tukio hilo lilitokea Februari 14, mwaka huu (Valentine’s Day) ambapo Shilole aliyekuwa amekwenda kufanya shoo mkoani humo, alishindwa kuzuia hisia zake baada ya mzazi mwenzake huyo kujitokeza na kujikuta wakioneshana mahaba mbele za watu.
Pozi hilo la kimahaba liliwashangaza watu na kuanza kudhani kuwa huenda wawili hao wakarudisha penzi lao lililokufa miaka mingi iliyopita.
“Mh! Kweli mtalaka hatongozwi, hebu ona Shilole alivyorembua alipomuona jamaa yake, pale Makala kumchukua ni kama kumsukuma mlevi,” alisema shuhuda mmoja.
Baada ya paparazi wetu ‘kuusoma mchezo’ huo, aliamua kumuuliza staa huyo kama penzi lao limerudi upya au laa?
“Hahahahaa! Kwa kweli unanichekesha kuniuliza kama nimerudisha penzi kwa mzazi mwenzangu, huyu ni baba wa mwanangu Joyce, itabaki kuwa hivyo. Siwezi kumtenga na sioni ajabu kupiga naye picha, hakuna kinachoendelea,’’ alisema Shilole.
Licha ya kufafanua hivyo, usiku wa siku hiyo, Shilole alipokuwa jukwaani akipagawisha mashabiki kwa shoo kali, alimpandisha jukwaani mzazi mwenziye huyo hali iliyozua mtafaruku mkubwa kwa mpenzi wa sasa wa Makala aliyefahamika kwa jina la Maguno.
Baada ya shoo kuisha, Maguno aliyekuwa na jazba kwa mpenzi wake kupandishwa jukwaani, alimsaka Shilole kwa udi na uvumba kutaka kumtembezea kichapo lakini bahati haikuwa yake, hakuweza kumpata hadi msanii huyo aliporejea jijini Dar siku iliyofuata

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname