AKIHOJIWA na CNN nchini Uingereza hivikaribuni wakati akihudhuria mkutano uliolenga kuongeza mapambano dhidi ya
ujangili,
Rais Jakaya Kikwete amepigilia msumari wa moto akisema Tanzania haiko
tayari kukubaliana na matakwa ya baadhi ya nchi za magharibi zinazotaka
nchi za Afrika ziwe na sheria zinazoruhusu ushoga.
"Itachukua
muda kwa watu wetu kukubaliana na tamaduni za watu wa magharibi,
nakumbuka Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron aliwahi kuzungumza sana
kuhusu suala hilo na likaleta shida na tafrani kubwa kwa watu wetu,"
alisema.
"nafikiri kwa watu wetu sidhani kama huu ni muda muafaka
wa kujadili suala hilo,hatulitaki na halikubaliki" alisema alipokuwa
akihojiwa na mtangazaji wa CNN, Christiane Amanpour.
Amannpour
alitaka kujua msimamo wa Rais Kikwete kuhusu haki za mashoga na harakati
zinazofanywa ili kuufaya ushoga kama moja ya haki za msingi za binadamu
No comments:
Post a Comment